Kanisa Kuu la
Waadventista la Wasabato la Kamunyonge katika Jimbo la Mara limewapata viongozi
wake wapya watakaoliongoza kanisa kwa mwaka 2015 huku majina kadhaa yakipanda
kwenye nyadhifa za juu na mengine kuhama nafasi moja kwenda nyingine.
Kwa mujibu wa taarifa
ya baraza la uchaguzi, aliyekuwa Katibu wa Kanisa kwa miaka mitatu mfululizo
Davis Mafuru amepanda na kuwa miongoni mwa Wazee watano watakaoshika hatamu
hapo mwakani wakati Mkuu wa Majengo wa 2014 Josiah Magomere akirejea tena kuwa
Mzee wa kanisa baada ya kushika wadhifa huo kwa vipindi tofauti tofauti hadi
2013.