Kanisa Kuu la
Waadventista la Wasabato la Kamunyonge katika Jimbo la Mara limewapata viongozi
wake wapya watakaoliongoza kanisa kwa mwaka 2015 huku majina kadhaa yakipanda
kwenye nyadhifa za juu na mengine kuhama nafasi moja kwenda nyingine.
Kwa mujibu wa taarifa
ya baraza la uchaguzi, aliyekuwa Katibu wa Kanisa kwa miaka mitatu mfululizo
Davis Mafuru amepanda na kuwa miongoni mwa Wazee watano watakaoshika hatamu
hapo mwakani wakati Mkuu wa Majengo wa 2014 Josiah Magomere akirejea tena kuwa
Mzee wa kanisa baada ya kushika wadhifa huo kwa vipindi tofauti tofauti hadi
2013.
Wazee wengine ni
pamoja na Emmanuel Sabayi aliyerejeshwa katika wadhifa huo baada ya kuutumikia
kwa vipindi tofauti hadi mwaka 2010,Nuhu Kigua anayeendelea kwa miaka mitatu
sasa sambamba na Selemani Wambura ambape pia amewahi kushika wadhifa huo katika
miaka ya hivi karibuni.
Baada ya kuiongoza idara
ya Uwakili kwa miaka mitatu mfululizo, Mkuu wa idara hiyo Asheri Mukama sasa anahamia idara ya Majengo iliyoachwa wazi
na Josiah Magomere aliyepanda kuwa Mzee
wa kanisa ambapo idara ya Shule Sabato itaendelea kuwa chini ya
Mkurugenzi wake Peter Robert Mugusi
Sogoto mbaye pia atakuwa Katibu wa idara ya Majengo.
Mkuu wa Majengo wa
mwaka 2011 hadi 2013 na Mkuu wa Miradi ya Kwaya ya Kanisa kwa mwaka huu wa
2014, Bigambo Jeje amepewa kuongoza idara mbili za Taaluma na Wajasiriamali (ATAPE)
sambamba na ile ya Mawasiliano kama mkuu wa idara hizo kwa mwaka 2015.
Aliyekuwa Mkuu wa
Mawasiliano mwaka huu Theodori John amepanda kuwa Katibu wa kanisa kuchukua
nafasi ya Mafuru aliyekuwa miongoni mwa Wazee wakati Katibu wa idara ya Uwakili
kati ya 2012 na 2014 Wema Nyakutonya anaenda kuongoza idara za Wana wa Kike na
Walemavu huku Diana Nico akipanda kuwa Shemasi Mkuu wa Kike akisaidiana na
mkongwe wa idara hiyo Yohana Chiama aliyerejea kushika wadhifa wa Shemasi Mkuu
wa Kiume.
Baraza hilo la
uchaguzi limemchagua Nashon Otieno maarufu kwa jina la “Wakudumu” aliyeongoza
kanisa hilo katika nyadhifa mbalimbali tangu mwaka 1982 kwenda kuongoza idara
ya Uwakili ilyoachwa wazi na Asheri Mukama huku nafasi yake ya idara ya Huduma
za kanisa anayomalizia mwaka huu ikishikwa na Elizabeth Joliga aliyehamishwa
toka idara ya Doricas.
Wengine waliochaguliwa
na nafasi zao zikiwa kwenye mabano ni Asheri Mukama (Mkuu wa Kwaya), Epaineto
Mujaya (Muziki), Pharesi Kauswa anayeendelea kuwa Mweka Hazina wa Kanisa, Mashaka
Nyangero Lugembe(Mazingira), Monica Sauli (idara ya Uchapaji) Joyce Mujungu
(Uinjilisti).
MWISHO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni