Pichani kulia ni Mwenyekiti wa halmshauri ya wilaya ya Serengeti Bw. John Ng'oina akiendesha kikao cha baraza hapo jana na kushoto ni Mkurugenzi wa halmshauri hiyo Bi Good Pamba (Picha Na Bigambo Jeje)
Picha ya Maktaba ya Waziri Nyalandu.
Rais Jakaya Kikwete anayeombwa amtimue Nyarandu
Na Bigambo
Jeje,Serengeti.
Kambi ya upinzani ya baraza la madiwani wa halmashauri ya
wilaya ya Serengeti mkoani Mara imemtaka Rais Jakaya Kikwete kumfukuza kazi
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe: Lazaro Nyarandu baada ya Waziri huyo kupingana na
ahadi ya Rais ya kujengwa kwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mugumu.
Kambi hiyo ikiongozwa
na msemaji wake Bw.Tanu Mwita amesema hatua hiyo ya kumpinga Rais Kikwete juu ya
ujenzi huo wa ndege wa kimataifa inatosha kabisa kuvuliwa wadhifa wake kwa kile
alichodai ni sawa na kuhujumu kiuchumi Watanzania hususani wananchi wa
Serengeti na mkoa wa Mara kwa ujumla sanjari na kukiuka kiapo cha utii kwa mkuu
wake wa kazi.
Bw.Tanu ambaye ni diwani
wa kata ya Kisangura amesema kauli ya hivi karibuni ya Waziri Nyarandu ya
Novemba mosi mwaka huu kupitia baadhi ya vyombo vya habari ni ya kutaka
kurudisha nyuma maendeleo ya kukuza sekta ya utalii na uchumi wa taifa hili
linalopiga hatua za kimaendeleo.
Kauli hiyo imetolewa
wakati baraza la madiwani la halmshauri hiyo likijadili ajenda ya kupokea hati
ya kuruhusu ujenzi wa uwanja huo wa ndege wa kimataifa unaotarajiwa kujengwa
kwa msaada wa kampuni ya uwekezaji ya Singita Grumet toka nchini Marekani
iliyowekeza katika sekta ya utalii ndani ya hifadhi ya wanyama ya Serengeti.
Kwa upande wake
mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya
Serengeti Bw. John Ng’oina amesema kuwa
wamekabidhiwa hati hiyo kwa kulazimisha kwani Waziri Nyarandu alikataa kwa
madai kuwa haiwezekani kujengwa kiwanja cha ndege katika mbuga na kwamba hata
kama wakijenga hatahakikisha ndege hazitui.
Bw. Ng’oina amesema
kauli hiyo ya Nyarandu aliitoa wakati alipohojiwa na gazeti la East Africa la
Novemba mosi mwaka huu akisema uwanja huo unajengwa umbali wa km 40 tokaa
hifadhi ya Serengeti jambo lisilowezekana kisheria lakini hiyo ilikuwa ni
kuwahadaa Watanzania kwa vile umbali wa kutoka hifadhini hadi eneo la uwanja ni
km 70.
“ Rais anasimama
anasema kiwanja cha ndege kitajegwa kwa gharama zozote,Waziri wake anasimama
anapinga, hii kweli ni akili” alihoji Ng’oina
na kushangiliwa na madiwani wa baraza hilo huku baadhi yao wakipaza
sauti wakisema afukuzwe kazi maana ameonekana msaliti na wengine wakiwataka
viongozi wa dini kumwombea kwa kile walichodai amelewa madaraka.
Bw. Ng’oina alisema wao
kama halmashauri wanayo dhamana ya kuhoji, kudai na kutetea haki yao kama
viongozi waliochaguliwa na wananchi, na kwamba hakuna halmashauri nchi hii
yenye kiwanja cha ndege,ila kuna baadhi
ya viongozi wachache ambao walikuwa hawaitakii mema halmashauri na
kuyapuuza madai kuwa endapo kiwanja cha ndege kitajengwa wanyama kama
nyumbu watatoka mimba kutokana na mlio wa ndege jambo ambalo si kweli.
Aidha Madiwani wa
halmashauri hiyo wamempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kutekeleza ahadi yake ya
ujenzi wa kiwanja cha ndege huku Jumanne Kwiro,Makamu Mwenyekiti wa halmashauri
hiyo akisema madiwani kwa pamoja wanalaani vikali kitendo cha Waziri Nyarandu kupinga maendeleo kwa kukataa ujenzi wa
kiwanja cha ndege licha ya kutowahi kufika wilayani Serengeti.
MWISHO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni