Ijumaa, 25 Julai 2014

WANAHABARI TANZANIA UNDENI CHAMA CHA WAFANYAKAZI

washiriki wa mafunzo ya intaneti mkoani Mara  wakipata kifungua kinywa  julai,24,2014.

Waandishi wa habari hapa nchini wametakiwa kuunda chama cha kitaifa cha kutetea haki za waandishi wa habari kama vilivyo vyama vya wafanyakazi vya CWT,TALGWU,TUGHE, TAMICO na vinginevyo ili kiweze kudai na kutetea haki na maslahi ya wanahabari.

Kauli hiyo imetolewa na Mwandishi Mwandamizi,Bigambo Jeje wakati wa mjadala wa mafunzo ya uandishi wa habari kwa Mtandao yaliandaliwa na Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika)MISA-TAN) yanayowashirikisha wanahabari wa Mkoa wa Mara.

Amesema kuwa wamiliki wa vyombo vya habari ni wanyonyaji wanapenda kuwatumia waandishi kwa habari lakini endapo kunatokea tatizo kwa mwandishi wao hawamsaidii na kudai kuwa hawamfahamu.

Akitoa mfano wa Marehemu, Daudi Mwangosi alipofariki chombo chake kilimkana kuwa yeye si mwajiriwa wa chombo hicho, na wakati alikitumikia chombo hicho kwa takribani miaka 10.

Ameiomba Wizara ya habari Utamaduni na Michezo kuangalia uwezekano wa kuwasaidia ,waandishi wa habari kwa kuwakutanisha wamiliki wa vyombo vya habari na waandishi kuzungumzia matatizo yanayowakabili ili taaluma hiyo iweze kuheshimiwa kama zilivyo taaluma zingine.

Juu ya malipo ya baadhi ya vyombo vya habari,Bigambo Jeje amesema kuwa kuna baadhi ya vyombo vya habari kutoka Marchi hadi sasa hawajawalipa waandishi wao wa habari.

Amesema wanaharakati wa vyombo vya habari,wanapaswa kutetea waandishi wao katika maslahi.

Jukwaa la wahariri linapaswa kusema waandishi wa habari wanaumia na kuweka msisitizo juu ya malipo yao lakini wamekuwa hawatetei maslahi ya waandishi hasa walioko Mikoani.

“Tunaweza kugoma kuandika habari kwenye vyombo vyetu ili vyombo vichukue hatua ya malipo kwetu” Amesema Jeje.
MUSOMA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni