Na Bigambo Jeje
Mwanasiasa mashuhuri toka Chama cha
Mapinduzi (CCM) mkoani Michael Mujinja amejitoa katika kinyang’anyiro cha
ubunge kupitia chama hicho katika jimbo la Musoma Vijijini huku akisema amejiondoa baada ya kujipima na
kuona hana rekodi za uchapazi na utendaji kama alionao Waziri wa zamani wa Nishati
na Madini Profesa Sospiter Muhongo anayewania ubunge wa jimbo hilo.
Mujinja ametoa uamuzi huo mjini hapa
alipokuwa akiongea na vyombo vya habari na kutanabaisha kwamba sasa anamuunga
mkono Profesa Muhongo ili apewe ridhaa ya kuwaongoza wananchi wa jimbo hilo
walio na kiu ya kupata maendeleo ya kweli katika Nyanja mbalimbali.
Amesema
baada ya kutafakari kwa kina amejiona pamoja na uwezo alionao lakini
bado hatoweza kufikia rekodi nzuri za uchapakazi alizonazo Profesa Muhongo
aliyetumikia nafasi ya Uwaziri kwa muda wa miaka 2 tu na kufanikiwa kusimamia
usambaji wa umeme vijijini nchi nzima na kuvuka lengo la urekelezaji wa ilani
ya CCM katika sekta hiyo kwa zaidi ya
asilimia 10 ya lengo lililokuwa limewekwa na chama hicho.
Amesema licha ya kuchangia maendeleo ya
jimbo hilo katika sekta za elimu na afya
kama mdau ikiwa ni pamoja na Zahanati ya kisasa katika kata ya Busambara katika
halmshauri ya wiaya ya Musoma Vijijini, amesema jimbo hilo kwa hivi sasa
linahitaji mtu mwenye maono na mipango
ya kuwavusha wananchi katika dimbi la umasikini na kuongeza kuwa anadhani
mwenye uwezo huo kwa hivi sasa ni Profesa Muhongo.
Kwa msingi huo amewashauri wagombea
ubunge wengine katika jimbo hilo kupitia CCM kufuata nyayo kama zake za
kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho ili kupisha nafasi kwa mgombea anayekubalika
na maelfu ya wananchi wa jimbo hilo ili watoe ridhaa ya ubunge kwa kiongozi
waliyemuomba ashirikiane nao katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.
Mbali na Profesa Muhongo, wagombea
wengine waliotangaza nia ya kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kupeperusha bendera ya
Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu ni pamoja na
Mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Anthony Mtaka, Profesa Tekere Mujungu
na Evarist Maganga.
MWISHO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni