Utekelezaji wa ahadi ya Rais Jakaya Kikwete, ya kumwachia mrithi wake mazingira ya kuongoza nchi tajiri, umeanza kutoa mwanga, ambapo Tanzania sasa inajiandaa kuongoza Afrika kwa kuwa na wataalamu wazawa wa mafuta na gesi.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
alitangaza kuwa katika miaka mitano ijayo, Tanzania itakuwa na wataalamu zaidi
ya 300, watakaokuwa wamebobea katika masuala hayo kutoka katika vyuo mbalimbali
vya kimataifa.