Pichani:Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi bibi Jenisita Mhagama
akiwasha mshumaa kwenye kaburi la Baba wa Taifa Mwitongo Butiama. (Na
Bigambo Jeje)
Na Bigambo Jeje,Butiama
Naibu wa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi Bibi Jenister Mhagama amewataka Watanzania kutowachagua viongozi
wanaochochea vurugu na fujo kwa wananchi, zenye nia ya kutowesha amani ya nchi
iliyoasisiwa na Baba wa Taifa marehemu Mwalimu Julius Nyerere wakati
tunapoelekea katika uchaguzi wa mkuu hapo mwakani.
Naibu Waziri Mhagama ametoa kauli hiyo
muda mfupi baada ya kuzulu kaburi la Marehemu Mwalimu Nyerere kijijini kwake
Mwitongo Butiama wilayani Butiama mkoani Mara ambapo alifuatana na viongozi wa
juu wa Chuo Kikuu Huria(OUT) wakiongozwa na Makamu Mkuu wa chuo hicho Profesa
Tolly Mbwete.