Na Bigambo Jeje,Musoma
JESHI la Polisi mkoani Mara
limesema,miili 36 kati ya 37 ya marehemu wa ajali iliyotokea Septemba 5 mwaka
huu eneo la Sabasaba na iliyohusisha
mabasi mawili ya Mwanza Coach na J4 Express na kujeruhi watu 80 imetambuliwa.
Kamanda wa Polisi mkoani Mara, Philipo
Kalangi amewambia wandishi wa habari ofisini kwake kuwa marehemu hao
wametambuliwa na ndugu zao isipokuwa mwili wa Charles Aloys pekee mwenye umri
wa miaka 37
Kalangi aliwataja maerehemu
waliotambuliwa kuwa ni watoto SylvesterAlphonce (2), Alberto Sylvester
(3)Fulgence Masinde (4) Mariamu Onesmo(5), Mashiku Ndiga(6 ) mkazi wa Nassa
Busega sanjari Ruhumbika Mafuru (7) mkazi wa Nyasho,Sabina Lawrance Masimo
(8) .
Wengine ni Kwesu Hamis Kaji mkazi wa
Iringo Musoma,Musa Masatu Masuke,Ramadhan Hamis,Jackson Kulomwa,Ibrahim Masatu
Nyashinda,Rebeka Mchinjo mkazi wa Mugango Butiama na Kasule Mashauri,Thabiti
Sharo,SaidAbdalah,Mamai Sombe,Kasule Mashauri na Frolence Malima.
Miili mingine ya marehemu waliotambuliwa
ni pamoja na Ramadhan Mrisho ambaye alikuwa kondakta wa basi la Mwanza
Coach,Ghati Ndege mkazi wa Kirumi mkazi wa Rorya, Ibrahim Hamis na Dk Anatoria Ntengeki
aliyekuwa Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Mara sambamba na Benardo Enyasi na mmoja
aliyetajwa kwa jina moja la Bonza.
Kamanda Kalangi amewataja marehemu zaidi
wa ajali hiyo ilyohusisha mabasi mawili kamba wamo pia Juma Sahi
Mambina,Jackson Kulondwa,Ernest Marwa,Magoti Juma,Salma Ibrahim mkazi wa Iringo
Musoma,Mwamini Ibrahim mkazi wa Mwisenge Musoma,Abdalah Musa,Mwikabi Kichibi na
Joshua Ruben aliyekuwa dereva wa basi la J4 Express.
Katika hatua nyingine Mganga mfawidhi wa
hospitali ya serikali mkoa wa Mara Dk Iragi Nzerageza amesema kuwa miili tisa
kati ya hiyo iliyotambuliwa bado imehifadhiwa katika chumba cha maiti
hospitalini hapo ikisubiri kuchukuliwa na ndugu na jamaa zao.
Dk Nzeregeza ameongeza kwamba marejeruhi
22 kati ya 80 waliopokelewa hospitalini hapo siku ya ijumaa muda mfupi baada ya
ajali, bado wamelazwa wakiendelea na matibabu huku hali zao zikiendelea vyema
ambapo wengine wameruhusiwa kufuatia hali zao kuimarika wakati baadhi yao
wamepelekwa hospitali ya rufaa ya Bugando ya Jijini Mwanza kwa matibabu zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni