Na Bigambo Jeje Musoma
Wagonjwa wanaoishi na virusi vya Ukimwi
toka mikoa mitatu ya Manyara,Mara na Kagera wapatao 23,000 wamekusanya
zaidi ya sh milioni 272 kutokana na
michango yao mbalimbali iliyowasaidia kujikimu kiuchumi sanjari na kupata
huduma za tiba na kinga kutokana na magonjwa nyemeleziyanayowakabili.
Katibu Tawala mkoa wa Mara Benedict Ole
Kuyan amepewa taarifa hiyo mjini hapa na Mkurugenzi wa Mpango wa shirika la kimataifa la AFRICARE hapa nchini
Tuntufye Mwakajonga wakati wa ufunguzi wa mkutano maalum wa kuhitimisha mradi
wa kutoa huduma za wagonjwa wa ukimwi majumbani.
Mwakajonga amesema fedha hizo
zilichangwa na wagonjwa hao wa ukimwi kati ya mwaka 2009 hadi mwezi Agosti mwaka huu kupitia mradi wa
Kaya CCI uliokuwa unatekelezwa na shirika hilo katika mikoa hiyo mitatu ambapo
zimewasaidia waathirika uweo kiuchumi kupitia uzalishaji wa huduma kuwekea na
vikundi vya mikopo vijijini.
Amesema kwa upande wa mkoa wa Mara
takwimu zinaonesha kuwa watu 10,524 wamefikiwa na mradi huo na kujikusanyia sh
milioni 204.7 kupitia vikundi vya VIKOBA 82 vilivyoanzishwa katika kipindi
hicho cha miaka mitano huku mikoa ya Kagera na Manyara ikwa na walengwa 12,474
na makusanyo yao yakifikia sh. milioni 67.3
Amezitaja changamoto walizokabiliana
nazo wakati wa utekelezaji wa mradi huo kuwa ni pamoja na ubaini wa uwepo wa
unyanyasaji wa kijinsia katika jamii,kubainika kwa kuongezeka kwa ukatili wa
kijinsia mkoani Mara kwa asilimia 66.4 zinazosababisha akina mama kushindwa
kupata huduma sambamba na halmshauri za wilaya kutenga bajeti kidogo za
kuwahudumia wagonjwa wa nyumbani.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoani
Mara Ole Kuyan ameziagiza halmashauri za wilaya mkoani hapa kuhakikisha
zinatenga fedha za kutosha katika bajeti zao ikiwa ni pamoja na halmshauri
ya wilaya ya Tarime kuanza mara moja
kuona umuhimu huo baada ya muda wote kutotenga kabisa bajeti ya aina hiyo
huduma za wagonjwa wa nyumbani.
MWISHO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni