Jumatatu, 17 Agosti 2015

Mathayo avunja ukimya na kumkana Lowassa






Na Bigambo Jeje


Hatimaye swahiba zamani wa karibu kisiasa wa mgombea urais wa UKAWA Edward Lowassa, Vedastus Mathayo amevunja ukimya na kuutangazia umma kwamba yeye na Lowassa urafiki wao kisiasa ulikoma tu pale alipohama CCM na kwenda CHADEMA.

Aidha amekanusha uvumi uliokuwa umetanda kwamba angeweza kuhamia CHADEMA kumfuata Lowassa kutokana na ukaribu wa kisiasa waliokuwa nao hususani katika kinyang’anyiro cha kura ya maoni ya Urais wa CCM na badala yake akawataka wana Mara na Watanzania kwa ujumla kumchagua Mgombea Urais wa CCM Dk John Magufuli.

Jumatatu, 27 Julai 2015

MWANASIASA MJINJA AMPISHA MUHONGO UBUNGE MUSOMA VIJIJINI


Na Bigambo Jeje
 
Mwanasiasa mashuhuri toka Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Michael Mujinja amejitoa katika kinyang’anyiro cha ubunge kupitia chama hicho katika jimbo la Musoma Vijijini  huku akisema amejiondoa baada ya kujipima na kuona hana rekodi za uchapazi na utendaji kama alionao Waziri wa zamani wa Nishati na Madini Profesa Sospiter Muhongo anayewania ubunge wa jimbo hilo.

Jumatatu, 26 Januari 2015

KABAKA ALIA NA VIONGOZI WA DINI KUHUSU AJIRA

                                                        Mhe: Joshua Mirumbe - Mkuu wa wilaya ya Bunda




Na Bigambo Jeje,Musoma.


Waziri wa Kazi na Ajira Mhe:Gaudensia Kabaka amewataka viongozi wa madhehebu ya dini kubuni miradi ya maendeleo katika taasisi za kidini wanazoziongoza ili kusaidia kupatikana kwa ajira katika sekta binafsi sanjari na kupunguza umasikini uliokithiri katika jamii hivyo kuisaidia serikali kutekeleza kwa vitendo dira ya taifa ya maendeleo.

Ijumaa, 23 Januari 2015

WAZIRI KABAKA KUONGOZA MAELFU YA WASABATO KAMUNYONGE






                                                   Pichani: Mhe Gaudensia Kabaka.




Waziri wa Kazi na Ajira Mhe:Gaudensia Kabaka January 25 mwaka huu anatarajia kuongoza maelfu ya waumini wa  kanisa la Waadventista la Wasabato la Kamunyonge la Musoma Mjini  ambalo ni kanisa Kuu la Wasabato jimbo la Mara, katika sherehe maalum ya kwaya ya kanisa hilo (Choir day) itakayofanyika katika viwanja vya kanisa hilo.

Jumanne, 6 Januari 2015

ZAHANATI YA MWIRINGO KUWANUFAISHA WATU 4000 KIAFYA



Bigambo Jeje,Musoma

Wananchi zaidi ya 4000 wa vijiji vitatu vya kata ya Busambara katika halmshauri ya wilaya ya Musoma Vijijini mkoani Mara watanufaika na huduma za afya baada ya zahanati inayojengwa katika kijiji cha Mwiringo kwa gharama y ash. milioni 150 kukamilika siku chache zijazo.