Jumapili, 21 Agosti 2016

MUSOMA EXPRESS NA CATA MINING ZATOA MISAADA YA SH BILIONI 1.2 MUSOMA

Na Bigambo Jeje,Musoma.
Agosti 3 2016.
MISAADA.

Pichani ni moja ya Mabasi mapya 18 ya kampuni ya Mabasi ya Musoma Express yanayotoa huduma za usafiri katika mikoa mbalimbali ya hapa nchini. 

Makampuni ya mabasi ya Musoma Express na Mgodi wa madini wa CATA uliopo wilaya ya Butiama mkoani Mara yametoa misaada ya zaidi ya sh bilioni 1.2 katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, kusaidia shughuli za maendeleo ya kijamii katika sekta mbalimbali kwa lengo la kupunguza umasikini na kukuza uchumi wa wananchi.

Jumatano, 3 Agosti 2016

MUSOMA KUMALIZA TATIZO LA MAJI KWA VIWANDA, WAWEKEZAJI




Imeandikwa na Bigambo Jeje
Imechapishwa: 03 Agosti 2016


MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Musoma (Muwasa) mkoani Mara inatarajia kuanza kuzalisha lita milioni 36 za maji kwa siku ifikapo Sepetemba mwaka huu hivyo kuwa na ziada ya lita milioni 12 za maji kila siku.

Hali hiyo inaipa uhakika wa huduma hiyo kwa wawekezaji mbalimbali wenye mahitaji makubwa ya maji. 

MIL. 200/- ZA MBUNGE MTAJI KWA WAJASIRIAMALI MUSOMA







WANAWAKE katika Manispaa ya Musoma mkoani Mara wamepata mikopo yenye thamani ya Sh milioni 200 itakayowasaidia katika shughuli za kiuchumi kupitia ujasiriamali.

Mikopo hiyo yenye riba nafuu imetolewa na Mbunge wa Musoma Mjini mkoani Mara kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Vedastus Mathayo, ikiwa ni utekelezaji wa moja ya ahadi alizozitoa kwa wananchi wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika Oktoba 25, 2015. 

Jumanne, 2 Agosti 2016

MRADI WA MAJI WALETA FARAJA BUNDA




Imeandikwa na Bigambo Jeje
Imechapishwa: 18 Januari 2016 

Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda akiweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Bunda katika kijiji cha Nyabehu mkoani Mara Machi 20, 2015. Wa pili kushoto ni aliyekuwa Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe na kushoto ni Mbunge wa Mwibara, Kange Lugora. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mara, Christopher Sanya, Mbunge wa zamani wa Bunda Stephen Wasira na Mkurugenzi wa kampuni ya Nyakirang’ani, Mauza Nyakirang’ani.  


KAMPUNI ya ujenzi ya Nyakirang’ani ya mjini Musoma mkoani Mara imeweza kutekeleza vyema mkataba wake na serikali wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyabehu wilayani Bunda ulioanza kutoa huduma kwa wananchi Oktoba 16, 2015.

Makala haya ya BIGAMBO JEJE inaelezea jinsi mradi huo ulivyoanza kunufaisha wakazi wa Bunda kiasi cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mara kuipongeza kampuni ya Nyakirang’ani kwa kufanikisha ujenzi huo kama mkataba ulivyotaka. 

KERO YA MAJI MUSOMA, BUNDA KUBAKI HISTORIA




Imeandikwa na Bigambo Jeje.
Imechapishwa: 06 Juni 2016 

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge akikata utepe kuzindua ujenzi wa tangi la maji kata ya Rwamlimi mjini Musoma


MAMIA ya maelfu ya wakazi wa Manispaa ya Musoma na wilaya ya Bunda mkoani Mara, siyo muda mrefu wataanza kunufaika na huduma ya maji safi na salama baada ya miradi ya maji kukamilika.

Miradi hiyo inatarajiwa kuzinduliwa kati ya Juni na Julai mwaka huu, hatua utakayomaliza kwa kiwango kikubwa kero ya upatikanaji wa maji salama takribani iliyodumu kwa muda mrefu.

MAJI NI UHAI,TUNZA MAZINGIRA YAKUTUNZE




Rais mstaafu Jakaya Kikwete akizindua mradi wa maji wa Mugumu katika hafla iliyofanyika kwenye bwawa la maji la Manchira wilayani Serengeti Julai 2, mwaka 2010.



Imeandikwa na Bigambo Jeje
Imechapishwa: 01 Julai 2016

WAFUGAJI kwenye baadhi ya vijiji katika wilaya ya Serengeti mkoani Mara wameiomba Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) kuwawekea vituo vya maji kunywesha mifugo ili kumaliza migogoro kati yao na wananchi wengine, wakiwemo wakulima.

HAPA KAZI TU IGUSE TAASISI ZILIZOLIMBIKIZA MADENI



Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo ya mradi huo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Musoma, Gantala Said, wakati wa sherehe za Kilele cha maadhimisho ya 27 ya Wiki ya Maji zilizofanyika Kitaifa Mkoani Mara jana Machi 22, 2015.

Imeandikwa na Bigambo Jeje.
Imechapishwa: 20 Januari 2016 

MAMLAKA ya Maji Safi na Taka ya Musoma Mjini (MUWASA) ni moja ya taasisi za umma ambazo kama zitalipwa ipasavyo na wadeni wake, zinaweza kuboresha utendaji kazi wake kuliko ilivyo sasa.

Wananchi wengi wa mji wa Musoma ambao wamekuwa wakilalamikia huduma ya maji, wamekuwa wakikutana na kauli ya ukata inayoisumbua mamlaka hiyo kutokana na kudai Sh milioni 560 ambazo hazijalipwa na baadhi ya Taasisi za Serikali mkoani Mara kutokana na taasisi hizo kulimbikiza ankra za huduma ya maji kwa muda mrefu.

MAKUSANYO YA NDANI YANUFAISHA MJI WA MUSOMA MARA MBILI



WATU waliowahi kuishi Musoma mjini, mkoani Mara miaka ya themanini hadi tisini na kisha kuondoka, bila shaka wana kumbukumbu ya mji uliokuwa msafi, ukiwa na barabara zisizotuamisha maji hata kama ni masika na barabara zenyewe ni za vumbi.