KATIBU wa Mila wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya,
Mwanasimtwa Mwagongo amesema tukio la kupatwa kwa jua linalotarajiwa kutokea
leo katika Kijiji cha Rujewa wilayani hapa ni ishara ya Mwenyezi Mungu
kuukubali uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli.
Alhamisi, 1 Septemba 2016
Jumapili, 21 Agosti 2016
MUSOMA EXPRESS NA CATA MINING ZATOA MISAADA YA SH BILIONI 1.2 MUSOMA
Na Bigambo Jeje,Musoma.
Agosti 3 2016.
MISAADA.
Pichani ni moja ya Mabasi mapya 18 ya kampuni ya Mabasi ya Musoma Express yanayotoa huduma za usafiri katika mikoa mbalimbali ya hapa nchini.
Makampuni ya mabasi
ya Musoma Express na Mgodi wa madini wa CATA uliopo wilaya ya Butiama mkoani
Mara yametoa misaada ya zaidi ya sh bilioni 1.2 katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, kusaidia shughuli za maendeleo
ya kijamii katika sekta mbalimbali kwa lengo la kupunguza umasikini na kukuza
uchumi wa wananchi.
Jumatano, 3 Agosti 2016
MUSOMA KUMALIZA TATIZO LA MAJI KWA VIWANDA, WAWEKEZAJI
Imeandikwa na Bigambo Jeje
Imechapishwa: 03 Agosti 2016
MAMLAKA
ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Musoma (Muwasa) mkoani Mara inatarajia
kuanza kuzalisha lita milioni 36 za maji kwa siku ifikapo Sepetemba mwaka huu
hivyo kuwa na ziada ya lita milioni 12 za maji kila siku.
Hali
hiyo inaipa uhakika wa huduma hiyo kwa wawekezaji mbalimbali wenye mahitaji
makubwa ya maji.
MIL. 200/- ZA MBUNGE MTAJI KWA WAJASIRIAMALI MUSOMA
WANAWAKE
katika Manispaa ya Musoma mkoani Mara wamepata mikopo yenye thamani ya Sh
milioni 200 itakayowasaidia katika shughuli za kiuchumi kupitia ujasiriamali.
Mikopo
hiyo yenye riba nafuu imetolewa na Mbunge wa Musoma Mjini mkoani Mara kupitia
tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Vedastus Mathayo, ikiwa ni utekelezaji wa
moja ya ahadi alizozitoa kwa wananchi wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa
Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika Oktoba 25, 2015.
Jumanne, 2 Agosti 2016
MRADI WA MAJI WALETA FARAJA BUNDA
Imeandikwa na Bigambo Jeje
Imechapishwa: 18 Januari 2016
Waziri
Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda akiweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Bunda
katika kijiji cha Nyabehu mkoani Mara Machi 20, 2015. Wa pili kushoto ni
aliyekuwa Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe na kushoto ni Mbunge wa
Mwibara, Kange Lugora. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mara, Christopher Sanya,
Mbunge wa zamani wa Bunda Stephen Wasira na Mkurugenzi wa kampuni ya
Nyakirang’ani, Mauza Nyakirang’ani.
KAMPUNI
ya ujenzi ya Nyakirang’ani ya mjini Musoma mkoani Mara imeweza kutekeleza vyema
mkataba wake na serikali wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyabehu wilayani Bunda
ulioanza kutoa huduma kwa wananchi Oktoba 16, 2015.
Makala
haya ya BIGAMBO JEJE inaelezea jinsi mradi huo ulivyoanza kunufaisha wakazi wa
Bunda kiasi cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mara kuipongeza kampuni ya
Nyakirang’ani kwa kufanikisha ujenzi huo kama mkataba ulivyotaka.
KERO YA MAJI MUSOMA, BUNDA KUBAKI HISTORIA
Imeandikwa na Bigambo Jeje.
Imechapishwa: 06 Juni 2016
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge akikata utepe kuzindua ujenzi wa tangi la
maji kata ya Rwamlimi mjini Musoma
MAMIA
ya maelfu ya wakazi wa Manispaa ya Musoma na wilaya ya Bunda mkoani Mara, siyo
muda mrefu wataanza kunufaika na huduma ya maji safi na salama baada ya miradi
ya maji kukamilika.
Miradi
hiyo inatarajiwa kuzinduliwa kati ya Juni na Julai mwaka huu, hatua
utakayomaliza kwa kiwango kikubwa kero ya upatikanaji wa maji salama takribani
iliyodumu kwa muda mrefu.
MAJI NI UHAI,TUNZA MAZINGIRA YAKUTUNZE
Rais mstaafu Jakaya
Kikwete akizindua mradi wa maji wa Mugumu katika hafla iliyofanyika kwenye
bwawa la maji la Manchira wilayani Serengeti Julai 2, mwaka 2010.
Imeandikwa na Bigambo Jeje
Imechapishwa: 01 Julai 2016
WAFUGAJI
kwenye baadhi ya vijiji katika wilaya ya Serengeti mkoani Mara wameiomba
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) kuwawekea vituo vya
maji kunywesha mifugo ili kumaliza migogoro kati yao na wananchi wengine,
wakiwemo wakulima.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)


