Imeandikwa na Bigambo Jeje
Imechapishwa: 18 Januari 2016
Waziri
Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda akiweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Bunda
katika kijiji cha Nyabehu mkoani Mara Machi 20, 2015. Wa pili kushoto ni
aliyekuwa Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe na kushoto ni Mbunge wa
Mwibara, Kange Lugora. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mara, Christopher Sanya,
Mbunge wa zamani wa Bunda Stephen Wasira na Mkurugenzi wa kampuni ya
Nyakirang’ani, Mauza Nyakirang’ani.
KAMPUNI
ya ujenzi ya Nyakirang’ani ya mjini Musoma mkoani Mara imeweza kutekeleza vyema
mkataba wake na serikali wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyabehu wilayani Bunda
ulioanza kutoa huduma kwa wananchi Oktoba 16, 2015.
Makala
haya ya BIGAMBO JEJE inaelezea jinsi mradi huo ulivyoanza kunufaisha wakazi wa
Bunda kiasi cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mara kuipongeza kampuni ya
Nyakirang’ani kwa kufanikisha ujenzi huo kama mkataba ulivyotaka.