washiriki wa mafunzo ya intaneti mkoani Mara wakipata kifungua kinywa julai,24,2014.
Waandishi
wa habari hapa nchini wametakiwa kuunda chama cha kitaifa cha kutetea haki za
waandishi wa habari kama vilivyo vyama vya wafanyakazi vya CWT,TALGWU,TUGHE,
TAMICO na vinginevyo ili kiweze kudai na kutetea haki na maslahi ya wanahabari.
Kauli hiyo imetolewa na Mwandishi Mwandamizi,Bigambo Jeje wakati wa mjadala wa
mafunzo ya uandishi wa habari kwa Mtandao yaliandaliwa na Taasisi ya vyombo vya
habari Kusini mwa Afrika)MISA-TAN) yanayowashirikisha wanahabari wa Mkoa wa
Mara.
Amesema kuwa wamiliki wa vyombo vya habari ni wanyonyaji wanapenda kuwatumia
waandishi kwa habari lakini endapo kunatokea tatizo kwa mwandishi wao
hawamsaidii na kudai kuwa hawamfahamu.
Akitoa mfano wa Marehemu, Daudi Mwangosi alipofariki chombo chake kilimkana
kuwa yeye si mwajiriwa wa chombo hicho, na wakati alikitumikia chombo hicho kwa
takribani miaka 10.
Ameiomba Wizara ya habari Utamaduni na Michezo kuangalia uwezekano wa
kuwasaidia ,waandishi wa habari kwa kuwakutanisha wamiliki wa vyombo vya habari
na waandishi kuzungumzia matatizo yanayowakabili ili taaluma hiyo iweze
kuheshimiwa kama zilivyo taaluma zingine.
Juu ya malipo ya baadhi ya vyombo vya habari,Bigambo Jeje amesema kuwa kuna
baadhi ya vyombo vya habari kutoka Marchi hadi sasa hawajawalipa waandishi wao
wa habari.
Amesema wanaharakati wa vyombo vya habari,wanapaswa kutetea waandishi wao
katika maslahi.
Jukwaa la wahariri linapaswa kusema waandishi wa habari wanaumia na kuweka
msisitizo juu ya malipo yao
lakini wamekuwa hawatetei maslahi ya waandishi hasa walioko Mikoani.
“Tunaweza kugoma kuandika habari kwenye vyombo vyetu ili vyombo vichukue hatua
ya malipo kwetu” Amesema Jeje.
MUSOMA.
Waandishi wa habari hapa nchini wametakiwa kuunda chama cha kitaifa cha kutetea
haki za waandishi wa habari kama vilivyo vyama vya wafanyakazi vya
CWT,TALGWU,TUGHE, TAMICO na vinginevyo ili kiweze kudai na kutetea haki na
maslahi ya wanahabari.